Ratiba ya Simba kuelekea Simba Day

Leo tumezindua rasmi ratiba yetu yetu ya wiki nzima kuelekea Tamasha la Kimataifa la Simba Day ambalo litafanyika Agoati 8 Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kama ilivyo kawaida yetu wiki moja kabla ya kilele cha Simba Day tunakuwa na matukio mbalimbali ya shuguli za kijamii.

Kesho Agosti Mosi tutakuwa na shughuli ya kusaini mkataba na mdhamini Mkuu M-BET.

Jumanne tutakuwa na zoezi la usafi kwa taasisi mbalimbali nchi nzima.

Jumatano itakuwa zoezi la kuchangia Damu nchi nzima

Ijumaa tunaenda kutembelea Magereza ya Watoto nchi nzima.

Jumamosi  wachezaji watapewa semina ya mambo mbalimbali ya kijamii.

Jumapili Dua.

Viingilio vya Tamasha letu vitakuwa kama ifuatavyo

Mzunguko Sh. 5000

Viti vya Orange Sh. 10,000

VIP B na C Sh. 20,000

VIP A Sh. 30,000

Platinum Sh. 200,000

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER