Rasmi tutakutana na Power Dynamos hatua ya pili Ligi ya Mabingwa

Mabingwa wa Zambia, Power Dynamos tutakutana nao katika hatua ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufanikiwa kusonga mbele kwa kuitoa African Stars ya Namibia.

Power Dynamos imevuka hhatua hiyo baada ya matokeo ya jumla ya 2-2 dhidi ya African Stars huku faida ya bao la ugenini ikiwabeba.

Simba ni miongoni mwa timu nane zinazoanzia hatua ya pili kutokana na idadi ya alama nyingi tulizokusanya kwenye viwango vya CAF.

Mchezo wa kwanza utapigwa nchini Zambia kati ya Septemba 15-17 wakati ile ya marudiano itapigwa jijini Dar es Salaam kati ya Septemba 29-30.

Ikumbukwe Power Dynamos tumekutana nao kwenye kilele cha Simba Day, Agosti 6 mwaka huu na kuibuka na ushindi mabao 2-0.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER