Klabu yetu imefanikiwa kuinasa saini ya mlinzi wa kati, Mohammed Ouattara kutoka Klabu ya Al Hilal ya Sudan kwa mkataba wa miaka miwili
Ouattara mwenye (23), raia wa Ivory Coast ni miongoni mwa chaguo la Kocha Zoran Maki ambaye wamewahi kufanya kazi pamoja nchini Sudan katika Klabu ya Al Hilal
Tayari Ouattara ameshajiunga na kikosi chetu Nchini Misri kinachoendelea na kambi ya maandalizi kwa ajili ya msimu ujao wa Mashindano 2022/23.
Mohammed Ouattara ni mlinzi mwenye uzoefu na soka la Afrika akiwa ameshacheza Wydad Athletic Club ya Morocco.