Rais Samia awapongeza Simba Queens

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan ameipongeza timu yetu ya Simba Queens baada ya kutwaa ubingwa wa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).

Queens imeshinda taji hilo jana baada ya kuifunga SHE Corporates kutoka Uganda bao moja katika mchezo wa fainali uliopigwa Uwanja wa Azam Complex.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais Samia ametuma salamu za pongezi na kututakia heri katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake itakayofanyika nchini Morocco.

“Nawapongeza wanangu wa Simba Queens kwa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kwa Wanawake (SAMIA CUP). Mmejenga heshima kwa soka la Tanzania na nchi kwa ujumla.

“Nawatakia kheri katika Ligi ya Mabingwa Afrika (2022 CAF Women’s Champions League) itakayofanyika nchini Morocco,” ameandika Rais Samia.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER