Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pongezi kwa klabu baada ya kufanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika.
Rais Samia ametuma salamu hizo kupitia ukurasa wake wa Twitter akionyesha kuthamini kazi kubwa tuliyofanya ya kuingia hatua na kupeperusha vema bendera ya nchi.
Katika salamu hizo, Rais Samia ameandika:
“Kongole Simba kwa ushindi wa bao 1-0 (ushindi wa jumla 4-1) mlioupata dhidi ya Premiero De Agosto ya Angola na kufanikiwa kuingia hatua ya makundi ya Klabu Bingwa barani Afrika. Nawatakia kila la kheri katika michuano inayofuata.”