Katika kufanya mabadiliko makubwa ya kikosi kuelekea msimu mpya wa mashindano 2025/2026 timu yetu ya Simba Queens imewaacha wachezaji 11.
Mabadiliko hayo yanatokana na malengo tuliyojiwekea kuelekea msimu ujao hasa ukizingatia msimu uliopita tulishindwa kutetea ubingwa wetu.
Nyota hao wengi wao mikataba yao imemalizika huku wachache wakiondoka kutokana na makubaliano ya pande mbili.
Wachezaji hao ni Ritticia Nabbosa, Precious Christopher, Wincate Kaari, Asha Djafari na Gelwa Yonah.
Wengine ni Josephine Julius, Asha Rashid, Mary Saiki, Carolyene Rufa, Jackline Albert na Daniella Ngoyi.