Queens yavunja kambi, wachezaji wapewa mapumziko

Kikosi chetu cha Simba Queens kimevunja kambi na wachezaji wamepewa mapumziko huku wale walioitwa Timu ya Taifa (Twiga Stars) wakiwa wameruhusiwa kwenda kujiunga kwa ajili ya Michuano ya COSAFA.

Kambi hiyo imevunjwa baada ya kunyakua ubingwa wa Klabu Bingwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kwa kuifunga SHE Corporates kutoka Uganda mwishoni mwa juma lililopita.

Wachezaji watakuwa na mapumziko ya wiki mbili kabla ya kurejea mazoezini Septemba 15 kujiandaa na Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (2022 CAF Women’s Champions League) itakayofanyika nchini Morocco kuanzia katikati ya Oktoba hadi Novemba mwaka huu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER