Kikosi chetu cha Simba Queens kimezidi kujiimarisha baada ya kukamilisha usajili wa mshambuliaji mwingine, Topistar Situma.
Topistar anatokea Kikosi cha Vihiga Queens ambao ndiyo mabingwa wa ligi kuu nchini kenya.
Msimu uliopita Topistar amefunga mabao 17 kwenye ligi ya Kenya akiwa ndiye mfungaji bora wa mashindano.
Topistar anakuwa usajili wa nne ndani ya kikosi cha Queens baada ya Zainabu Mohamed, Ibinabo Alex kutoka Nigeria na Philomena Abakah kutoka Ghana.
Tunaendelea kuimarisha kikosi chetu kuelekea msimu ujao wa ligi pamoja na michuano ya CECAFA ambayo itaanza mwisho wa mwezi huu jijini Arusha.