Simba Queens imepoteza mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania (TWPL) baada ya kufungwa bao moja dhidi ya Yanga Princess katika mchezo uliopigwa Uwanja wa KMC Complex.
Mchezo ulianza kwa kasi huku timu zote zikishambuliana kwa zamu lakini ufanisi wa kutumia ulikuwa chini.
Jeannine Mukandayisenga aliipatia Yanga Princess bao hilo pekee dakika ya 47 kwa shuti kali la chini chini baada ya kupokea pasi kutoka kwa Adebisi.
Baada ya bao hilo Queens iliongeza kasi ya mashambulizi ya kutaka kusawazisha lakini Yanga walikuwa imara kuondoa hatari zote.
Kocha Yussif Basigi, alifanya mabadiliko ya kuwatoa Precious Christopher, Fatuma na Asha Issa kuwaingiza Elizabeth Wambui Asha Rashid na Ritticia Nabbosa.