Queens yapangwa kundi B michuano ya CECAFA

Timu yetu ya Simba Queens imepangwa kundi B katika michuano ya kufuzu fainali za Afrika kwa Wanawake kutoka Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).

Queens amepata tiketi ya kushiriki michuano hiyo kwa sababu imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania (TWPL) msimu uliopita.

Timu tisa zimepangwa kwenye makundi mawili na bingwa wa michuano hiyo ataiwakilisha CECAFA kwenye mashindano ya Afrika.

Kundi B ambalo ndio tupo lina timu zifuatazo:

Simba Queens (Tanzania)

PVP Buyenzi (Burundi)

Kawempe Muslim (Uganda)

Fad Djibouti (Djibouti)

Michuano hiyo itaanza kutimua vumbi Agosti 17 na kumalizika Septemba 4 katika mji wa Addis Ababa nchini Ethiopia.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER