Mchezo wetu wa Serengeti Lite Women’s Premier League dhidi ya watani wetu wa jadi Yanga Princess uliopigwa Uwanja wa Uhuru umemalizika kwa sare ya kufungana bao moja.
Mchezo ulianza kwa kasi huku timu zikishambuliana kwa zamu na kutengeza nafasi lakini ufanisi wa kuzitumia haukuwa mzuri.
Tulikuwa wakwanza kupata bao kupitia kwa Jentrix Shikangwa dakika ya 29 baada a Kupokea pasi ya kiungo Vivian Corazone.
Bao hilo lilidumu mpaka timu zinaenda mapumziko. Baada ya kurejea kasi ya mchezo iliendelea kuwa juu huku timu zikiendelea kupoteza nafasi ilizotengeneza.
Yanga Princess ilisawazisha bao hilo dakika ya 77 kupitia kwa Wogu Chioma kufuatia mpira mrefu uliopigwa kutoka pembeni na mlinda mlango wetu Gelwa Yona kushindwa kuukamata kabla ya kumkuta mfungaji.
Kocha mkuu, Charles Lukula alifanya mabadiliko ya kuwatoa Mwanahamisi Omary, Vivian Corazone na Asha Djafar na kuwaingiza Joelle Bukuru, Olaiya Barakat na Pambani Kuzoya.