Queens yaishushia mvua ya mabao Mlandizi

Simba Queens imefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 11-0 dhidi ya Mlandizi Queens katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake uliopigwa Uwanja wa KMC Complex.

Aisha Mnuka alitupatia bao la kwanza kwa kichwa dakika ya saba kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na mlinzi Ruth Ingosi.

Asha Djafar alitupatia bao la pili dakika ya 16 baada ya mpira uliopigwa na Jentrix Shikangwa kugongwa kwa kichwa na mlinzi wa Mlandizi kabla ya kumkuta mfungaji.

Ruth Ingosi alitupatia bao la tatu kwa kichwa dakika ya 22 baada ya kumalizia mpira wa kona uliopigwa na Precious Christopher.

Jentrix Shikangwa alitupatia bao la nne dakika ya 50 baada ya kumaliza pasi ndefu iliyopigwa kutoka katikati ya uwanja na Fatuma Issa.

Dakika mbili baadae Mnuka alitupia bao la tano baada ya kugongeana vizuri na Shikangwa ndani ya 18 na kupiga shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa Mlandizi.

Shikangwa alitupatia bao la sita dakika ya 56 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Mnuka.

Shikangwa alitupatia bao la saba dakika ya 60 kwa mkwaju wa penati baada ya mlinzi wa Mlandizi kuunawa mpira ndani ya 18 baada ya kupigwa chenga na Precious.

Precious Christopher alitupatia bao nane dakika ya 62 kwa shuti kali ndani ya 18 baada ya kumalizia pasi ya Shikangwa.

Djafari alitupatia bao tisa dakika ya 66 baada ya kumalizia pasi ndefu iliyopigwa na Vivian Corazone.

Dakika ya 78 Djafar alitupatia bao la kumi baada ya kupokea pasi ndefu kwa Ritticia Nabbosa huku Shikangwa alikamilisha la mwisho dakika ya 90.

Kocha Yussif Basigi alifanya mabadiliko ya kuwatoa Mnuka, Corazone, Djafar, Precious na Esther Mayala kuwaingiza Ritticia Nabbosa, Janeth Nyagali, Zawadi, Jackline Albert na Amina Bilal.

Matokeo hayo yanaifanya Queens kuendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa Ligi ikiwa na alama 28 baada ya kucheza mechi 10.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER