Queens yaisambaratisha The Tigers

Kikosi chetu cha Simba Queens kimefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya The Tigers katika mchezo wa Serengeti Lite Women’s Premier League uliopigwa Uwanja wa Black Rhino, Karatu.

Nahodha Opa Clement alitupatia bao la mapema dakika ya pili baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa The Tigers.

Bao hilo lilidumu mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika ingawa kulikuwa na mashambulizi ya pande zote lakini changamoto ikawa katika umaliziaji.

Pambani Kuzoya alitupatia bao la pili dakika ya 48 kabla ya kuongeza la tatu dakika ya 52.

Opa alikamilisha karamu ya mabao kwa kutupia la nne baada kuwazidi kasi walinzi wa Tigers na kuachia shuti la chini chini lililomshinda mlinda mlango.

Kocha Charles Lukula alifanya mabadiliko ya kuwatoa Vivian Corazone na Joelle Bukuru na kuwaingiza Fatuma Issa ‘Fetty Densa’, pamoja na Amina Ramadhani.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER