Timu yetu ya Simba Queens imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao moja dhidi ya JKT Queens katika muendelezo wa Ligi Kuu ya Wanawake (Serengeti Lite Womens Premier League) mchezo uliofanyika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuyo.
Mchezo huo ulikuwa mgumu kutokana na ubora wa timu zote na tulisuburi mpaka dakika ya 45 kupata bao la kwanza kupitia kwa Lionet Lioka aliyejifunga katika harakati za kuokoa.
Kipindi cha pili tuliendelea kushambuliana kwa zamu lakini hata hivyo matokeo yaliendelea kubaki kama awali.
Kocha Sebastian Nkoma alifanya mabadiliko ya kuwatoa Zubeda Mgunda, Jackline Albert na Pambani Kuzoya na kuwaingiza Olaiya Barakat, Amina Ramdhani na Mercy Tagoe.
Mei 20 mwaka huu, tutacheza mchezo wa mwisho wa kufungia msimu katika Uwanja wa Uhuru dhidi ya Baobab Queens ambao tutakabidhiwa taji letu la ubingwa.
Tunaendelea kuwasisitiza mashabiki wetu kujitokeza kwa wingi kusherehekea ubingwa ambao tumeutwaa kwa mara tatu mfululizo.