Kikosi cha Simba Queens kimeondoka asubuhi kuelekea jijini Dodoma kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania (TWPL) dhidi ya Gets Program utakaopigwa Jumatano Machi 26 katika Uwanja wa Jamhuri.
Queens imeondoka na jumla ya wachezaji 22 tayari kwa mchezo huo ambao kwa namna yoyote tunahitaji kupata alama tatu.
Mratibu wa timu, Selemani Makanya amesema wamejipanga vizuri kuhakikisha alama tatu zinapatikana huku akiamini bado tupo kwenye mbio za ubingwa.
“Tunaondoka kuelekea Dodoma kwa ajili ya mchezo wa Jumatano dhidi ya Gets Program, tumeondoka na kikosi cha wachezaji 22 ambao tunaamini watatuwezesha kufikia malengo yetu.
“Malengo yetu ni kuhakikisha tunapata alama tatu kwenye mchezo huo, tunahitaji kushinda kila mchezo ili kutetea ubingwa wetu,” amesema Makanya.