Queens yaichakaza Mlandizi Simba Day

Kikosi chetu cha Simba Queens kimefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 7-0 dhidi ya Mlandizi Queens katika mchezo wa kirafiki wa ufunguzi wa Simba Day.

Mchezo huo ulikuwa mzuri huku tukitawala sehemu kubwa na kufanya mashambulizi mengi langoni mwa Mlandizi.

Nyota wetu Precious Christopher alifungua akaunti yake ya mabao kwa kufunga bao la kwanza akiwa na kikosi chetu.

Mkongwe Asha Rashid ‘Mwalala’ aligunga mabao matatu ‘hat trick’ huku akionyesha kiwango bora.

Katika ushindi huo mnono Shelda Boniface alitupia mabao mawili huku Jentrix Shikangwa akifunga moja.

 

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER