Queens yaichakaza Geita Nyankumbu

Kikosi cha Simba Queens kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Geita Queens katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake uliopigwa Uwanja wa Nyankumbu.

Aisha Juma alitupatia bao la kwanza dakika ya 18 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Jentrix Shikangwa.

Mlinzi wa kati Ruth Ingosi alitupatia bao la pili baada ya kumalizia pasi ya Aisha Mnuka akiwa ndani ya 18.

Joanitah Ainembabazi alikamilisha karamu ya mabao kwa kufunga bao la tatu baada ya kumpiga chenga mlinda mlango wa Geita kufuatia kupokea pasi kutoka kwa Mnuka.

Kocha Msaidizi Mussa Hassan Mgosi alifanya mabadiliko ya kuwatoa Daniella Ngoyi, Shikangwa, Elizabeth Wambui na kuwaingiza Silvia Thomas, Joanitah Ainembabazi na Mwanahamisi Omary.

Simba Queens imefikisha pointi 25 ikiendelea kusalia kileleni mwa msimamo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER