Queens yaendeleza ushindi Ligi ya Wanawake

Simba Queens imezidi kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania TWPL baada ya kuifunga Mashujaa Queens mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Kituo cha TFF Kigamboni.

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku tukitawala sehemu kubwa na kufika zaidi langoni mwa Mashujaa lakini tulipoteza umakini.

Elizabeth Wambui alitupatia bao la kwanza dakika ya 10 kwa shuti kali baada ya kuunganisha pasi safi kutoka kwa Vivian Corazone.

Kipindi cha pili tuliongeza kasi huku tukifika zaidi langoni mwa Mashujaa huku wao wakifanya mashambulizi ya kushtukiza.

Wincate Kaari alitupatia bao la pili dakika ya 61 kwa mpira wa adhabu ulioenda moja kwa mojaa wavuni baada ya Elizabeth Wambui kufanyiwa madhambi nje ya 18.

Kocha Yussif Basigi alifanya mabadiliko ya kuwaingiza Dotto Evarist, Asha Rashid ‘Mwalala’, Ritticia Nabbosa, Mwanahamisi Omary na Emiliana Mdimu na kuwatoa Jentrix Shikangwa, Esther Mayala, Wincate, Elizabeth Wambui na Vivian Corazone.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER