Queens yaendeleza dozi ilipoishia

Timu yetu ya Wanawake Simba Queens imeendelea kukusanya alama tatu baada ya kuifunga Ilala Queens mabao 3-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake (Serengeti Lite Womens Premier League) uliopigwa Uwanja wa Mo Simba Arena.

Asha Djafar alitupatia bao la mapema zaidi dakika ya kwanza baada ya kuwazidi kadi walinzi wa Ilala Queens.

Bao hilo lilidumu mpaka tunaenda mapumziko licha ya mashambulizi mengi tuliyofanya kutokana na kushindwa kuzitumia vema nafasi tulizopata.

Jackline Albert alitupatia bao la pili dakika ya 48 akitumia udhaifu wa walinzi wa Ilala ambao walizembea kuondoa hatari.

Kiungo mshambuliaji Joelle Bukuru alikamilisha karamu ya mabao kwa kufunga la tatu dakika ya 90 baada ya mpira uliopigwa juu na kuunganisha moja kwa moja.

Kocha Sebastian Nkoma alifanya mabadiliko ya kuwatoa Olaiya Barakat na Amina Ramadhani kumuingiza Mercy Tagoe pamoja na Zubeda Mgunda.

Ushindi huo unatufanyia kufikisha pointi 45 tukiendelea kukaa kileleni mwa msimamo baada ya kucheza mechi 16.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER