Wachezaji wa Simba Queens jana na leo wamefanyiwa vipimo vya afya kabla ya kuanza maandalizi ya msimu mpya wa mashindano 2024/25.
Vipimo hivyo vimegawanyika katika sehemu kuu tatu ambayo ni damu, mapafu na moyo pamoja na kupima utimamu wa misuli na mishipa.
Queens itashiriki mashindano ya klabu bingwa kwa ukanda wa Afrika Mashariki (CECAFA) yanayotarajia kuanza Agosti 14 mwaka huu nchini Ethiopia.
Bingwa wa michauno hiyo anapata tiketi ya kushiriki mashidano ya klabu Bingwa Afrika.