Queens waanza na dozi kali CECAFA

Kikosi chetu cha Timu ya Wanawake cha Simba Queens kimeanza vema michuano ya Ligi ya Mabingwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) baada ya kuishushia dozi nzito Garde Publicaine FC ya Djibouti mabao 6-0.

Mchezo huo ulikuwa wa upande mmoja zaidi huku tukitawala sehemu na kufanya mashambulizi mengi.

Fallone Pambani alitupatia bao la kwanza dakika ya 30 kabla ya Olaiya Barakati kuongeza la pili dakika mbili baadae huku Asha Djafar akitupia la tatu na kutufanya kwenda mapumziko tukiwa mbele kwa mabao 3-0.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi ambapo dakika ya 51 Joelle Bukuru alitupatia bao la nne na Djafar kuongeza la tano dakika ya 68.

Olaiya alikamilisha karamu ya mabao kwa kufunga la sita likiwa na pili kwake katika mchezo wa leo baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Gerda.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER