Queens na JKT zagawana pointi KMC Complex

Mchezo wa wetu wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania (TWPL) dhidi ya JKT Queens uliopigwa Uwanja wa KMC Complex umemalizika kwa sare ya kufungana bao moja.

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku tukishambuliana kwa zamu lakini safu za ulinzi zulikuwa imara kuhakikisha mara zote wanakuwa salama.

Elizabeth Wambui alitupatia bao la kwanza dakika ya 47 kipindi cha kwanza kwa shuti kali akiwa ndani ya 18 baada ya kupokea pasi safi kutoka Vivian Corazone.

Kipindi timu zote zilirudi kwa kasi na huku zikishambuliana kwa zamu lakini umakini wa kutumia nafasi ilizopata ikawa changamoto.

Donisia Minja aliisawazishia JKT Queens bao hilo dakika ya 67 kwa mpira wa adhabu uliotinga wavuni moja kwa moja kufuatia madhambi yaliyofanywa karibu ya goli upande wa kushoto.

Baada ya matokeo hayo Simba Queens imeendelea kusalia kileleni mwa msimamo ikiwa na pointi 16 baada ya kucheza mechi 6 alama mbili zaidi ya JKT.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER