Queens mwendo mdundo

Timu yetu ya Wanawake Simba Queens imeendeleza ubabe katika Ligi Kuu ya Wanawake (Serengeti Lite Women’s Premier League) baada ya kuifunga Ruvuma Queens mabao 2-0.

Queens ilipata mabao hayo kwa haraka ndani ya dakika 12 na 14 yaliyofungwa na Asha Djafar na Amina Ramadhani.

Haukuwa ushindi rahisi kutokana na Ruvuma kutupa upinzani mkali lakini wachezaji wetu walikuwa makini kuhakikisha tunapata matokeo chanya.

Hata hivyo, tulikuwa na uwezo wa kupata ushindi mnono zaidi ya huo kama washambuliaji wetu wangeongeza umakini kwa kutumia vema nafasi tulizopata.

Ushindi wa leo unatufanya kuendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi tukifikisha pointi 36 baada ya kushinda mechi zote 12.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER