Queens kumaliza mzunguko bila kuangusha pointi

Kocha Mkuu wa Timu ya Simba Queens, Sebastian Nkoma ameweka wazi kuwa malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda mchezo wa kesho dhidi ya Fountain Gate ili kumaliza mzunguko wa kwanza bila kudondosha alama hata moja.

Mchezo wa kesho ambao utapigwa Uwanja wa Mo Simba Arena saa 10 jioni utakuwa wa 11 na utakuwa wa kumalizia mzunguko wa kwanza wa Serengeti Women’s Premier League.

Nkoma amesema mchezo utakuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda ili kukamilisha malengo ya kumaliza mzunguko bila kudondosha alama yoyote.

Kocha huyo mwenye uzoefu mkubwa katika medani ya soka amesema tutawakosa wachezaji kutoka nje ambao wanaenda kujiunga na timu zao za taifa lakini tuna kikosi kipana ambacho kinaweza kucheza mechi yoyote.

“Malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda mchezo wa kesho na kumaliza mzunguko bila kudondosha alama. Tumecheza mechi 10 na tumeshinda zote, tunataka na kesho tushinde.

“Tunajua mchezo utakuwa mgumu, pia tutawakosa baadhi ya wachezaji ambao wanaenda kujiunga na timu zao za taifa lakini tuna wachezaji wengi kikosini ambao wanaweza kutupa ushindi,” amesema Nkoma.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER