Droo ya michuano ya Samia Women’s Super Cup imekamilika na kikosi chetu cha Simba Queens kimepangwa na JKT Queens katika mchezo wa nusu fainali utakaopigwa katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Michuano hiyo ni Maalum kwa ajili ya kilele cha siku ya Wanawake Dunia ambayo inadhaminiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Saluhu Hassan.
Mchezo dhidi ya JKT utapigwa Machi 4 katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambapo mshindi atacheza na Yanga Princess au Fountain Gate Princess.
Kikosi cha Queens kinatarajia kuondoka wikiendi hii kuelekea Arusha tayari kwa ajili ya kushiriki michuano hiyo.