Kikosi chetu cha Simba Queens kesho kitashuka katika Uwanja wa Samora mkoani Iringa kuikabili Ceasiaa Queens katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania (TWPL).
Queens imewasili Iringa tangu jana na leo kikosi kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Samora tayari kwa mchezo huo utakaonza saa 10 jioni.
Wachezaji wote waliosafiri na timu wameshiriki mazoezi hayo na hakuna aliyepata maumivu ambayo yatamfanya kuukosa mchezo wa kesho.
Queens itaingia kwenye mchezo wa kesho ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 3-1 iliyopata dhidi ya Fountain Gate Princess kwenye mechi iliyopigwa na Oktoba 14.
Queens ndio vinara wa Ligi Kuu ya Wanawake ikiwa na alama sita ikifunga mabao sita na kuruhusu moja katika mechi mbili.