Queens ipo kamili kuivaa Bunda Queens

Kikosi chetu cha Simba Queens kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania (TWPL) dhidi ya Bunda Queens utakaopigwa kesho saa 10 jioni Uwanja wa Azam Complex.

Kikosi kimefanya mazoezi ya mwisho ya kujiandaa na mchezo huo na wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri.

Kocha Mussa Hassan Mgosi mara zote amekuwa akisema kuwa malengo yetu ni kushinda kila mchezo ulio mbele yetu.

Kila mchezo tumeupa umuhimu sawa na hatuwezi kudharau timu yoyote kwa sababu tunataka kurejesha taji letu ambalo tulilipoteza msimu uliopita.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER