Pointi moja ugenini

Kikosi chetu kimefanikiwa kupata alama moja ugenini dhidi ya US Gendarmerie Nationale ya Niger katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi uliopigwa Uwanja wa Jenerali Senyi Kountche nchini Niger.

Wenyeji Gendarmerie walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 12 lililofungwa na Gbeuli Wilfred baada ya kiungo Sadio Kanoute kuzembea kuondoa hatari.

Baada ya bao hilo tulirudi mchezoni na kufanya mashambulizi kadhaa langoni mwa Gendarmerie lakini tulikosa umakini kama walivyofanya wenyeji.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi na kulifikia zaidi lango la Gendarmerie huku wenyeji wakicheza nyuma na kutumia mipira mirefu.

Mlinzi Pascal Wawa ambaye aliingia dakika ya 45 kuchukua nafasi ya Joash Onyango alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumia na kutolewa nafasi yake ikachukuliwa na Kennedy Juma.

Bernard Morrison alitusawazishia bao hilo kwa kichwa dakika ya 83 baada ya kumalizia mpira wa kona uliopigwa na Shomari Kapombe.

Kocha Pablo Franco aliwatoa Joash Onyango, Yusuf Mhilu, Peter Banda, Erasto Nyoni na kuwaingiza Pascal Wawa, Morrison, John Bocco, Jimmyson Mwinuke.

Sare ya leo inatufanya kufikisha pointi nne baada ya mechi mbili huku tukiongoza kundi D.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER