Nyota watatu wameingia fainali ya kinyang’anyiro cha kumtafuta Mchezaji Bora wa Mashabiki wa Mwezi Septemba (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month).
Wachezaji hao ni mshambuliaji Moses Phiri, na viungo Clatous Chama na Mzamiru Yassin.
Kabla ya kubaki nyota hao watatu walioingia fainali ambapo kabla ya mchujo walikuwa watano akiwamo Mohamed Hussein na Augustine Okrah.
Takwimu za nyota wote mwezi Septemba
Mechi Goli Assist Dakika
Phiri 4 3 2 334
Chama 4 0 2 352
Mzamiru 4 0 0 328
Zoezi la kupiga kura kupitia tovuti yetu ya www.simba.co.tz limeanza rasmi leo Jumanne Septemba, 27 na litafungwa Septemba, 30 saa sita usiku.
Mshindi wa jumla atakabidhiwa fedha taslimu Sh 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium Profile.