Pablo: Ushindi dhidi ya ASEC ni muhimu sana kwetu

Kocha Mkuu Pablo Franco, amesema ushindi wa mabao 3-1 tuliopata jana dhidi ya ASEC Mimosas katika Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ni muhimu na umerudisha hali ya kujiamini kikosini.

Pablo amesema michuano ya Afrika mara zote ni vizuri kupata ushindi katika uwanja wa nyumbani ili ugenini ukipata hata sare inakuweka katika hali nzuri.

Akizungumzia mchezo wenyewe, Pablo amesema ulikuwa mgumu na wa kimbinu lakini tulikuwa bora zaidi yao kwenye kutengeneza nafasi na kumiliki mpira.

Pablo ameongeza kuwa tulikuwa na nafasi ya kupata ushindi mnono zaidi kama tungezitumia vizuri nafasi za wazi tulizopata kipindi cha kwanza ingawa hata hivyo amewapongeza wachezaji kwa kazi kubwa waliyofanya.

“Ni ushindi muhimu tumepata, tulicheza vizuri, tulitengeneza nafasi na tulikuwa na uwezo wa kushinda zaidi ya mabao tuliyopata. Kwanza niwapongeze wachezaji kwa kazi kubwa waliyofanya, haikuwa rahisi,” amesema Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER