Kocha Mkuu Pablo Franco, ameweka wazi kuwa mchezo wetu wa kesho dhidi ya Kagera Sugar utakuwa mzuri kuutazama sababu eneo la kuchezea (pitch) la Uwanja wa Kaitaba ni zuri.
Pablo amesema baada ya mechi kumalizika kila mtu atakuwa na nafasi ya kuzungumzia mchezo ulivyokuwa na si vinginevyo na mechi mbili zilizopita.
Raia huyo wa Hispania ameongeza kuwa mchezo utakuwa mgumu sababu Kagera ina kikosi imara na inacheza soka la moja kwa moja hivyo mechi itaamuliwa kwa mbinu zaidi.
“Tumekuja Kagera hii ni mara ya pili, mara ya kwanza mechi ilishindwa kufanyika sababu ya matatizo ya kiafya lakini tunaamini kesho itafanyika na tupo tayari kwa mapambano.
“Mchezo utakuwa mzuri hata kuutazama sababu sehemu ya kuchezea ni nzuri kwa hiyo kila timu itakuwa na uwezo wa kucheza tofauti na mechi zetu zilizopita,” amesema Pablo.
Pablo ameongeza kuwa; “Tunajua mechi itakuwa ngumu, Kagera ni timu nzuri inacheza soka safi na wapo kwenye kiwango bora sasa lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda.”
One Response