Kocha Mkuu Pablo Franco, amesema tutaingia katika mchezo wa kesho wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Gendarmerie Nationale kwa lengo la kutafuta alama tatu lakini ikishindikana tutapambana kupata walau moja.
Pablo amesema tutacheza kwa jitihada muda wote wa mchezo ili kuhakikisha tunafanikisha malengo ya kuchukua pointi zote tatu za ugenini.
Pablo ameongeza kuwa mchezo utakuwa mgumu sababu wenyeji Gendarmerie walipoteza mechi ya kwanza hivyo watajipanga kuhakikisha wanatumia vema uwanja wao wa nyumbani.
“Tutaingia katika mchezo wa kesho kwa lengo la kutafuta pointi tatu muhimu ugenini, tusipofanikiwa tutahakikisha tunatafuta sare lakini si kupoteza.
“Tunajua mchezo utakuwa mgumu, Gendarmerie wametoka kupoteza mechi ya kwanza na watataka kutumia vema uwanja wa nyumbani lakini tuko tayari kuwakabili,” amesema Pablo.
One Response