Pablo: Tunataka ushindi kwa ajili ya mashabiki wetu

Kocha Mkuu Pablo Franco ameweka wazi kuwa tunahitaji kupata ushindi katika mchezo wetu wa Jumapili wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Gandarmerie ili kuwapa furaha mashabiki wetu.

Pablo amesema anaamini mashabiki watajitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa hiyo itakuwa jambo zuri kushinda ili kusherehekea kwa pamoja.

Pablo raia wa Hispania ameongeza kuwa lengo la kwanza ni kuhakikisha tunashinda katika mchezo huo ambao ni kama fainali kwetu lakini pia kuonyesha kandanda safi la kuvutia mashabiki watakaojitokeza.

“Tunajua tunahitaji kushinda ili kuwapa furaha mashabiki wetu, naamini watajitokeza kwa wingi Jumapili hivyo ni jukumu letu kuhakikisha wanafurahi,” amesema Pablo.

Kikosi kimeingia kambini jana mchana na kufanya mazoezi jioni ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo huo.

SHARE :
Facebook
Twitter

3 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER