Kocha Mkuu Pablo Franco amesema sare dhidi ya Azam FC si matokeo tuliyokusudia kuyapata kwa kuwa tulihitaji kuondoka na alama zote tatu katika Uwanja wa Azam Complex.
Pablo amesema tuliingia katika mchezo huu tukiwa na lengo la kutafuta alama tatu ambazo zingetufanya kupunguza tofauti ya pointi iliyopo baina yetu na wanaongoza ligi.
Akiuzungumzia mchezo wenyewe Pablo amesema ulikuwa mgumu na tulitarajia ungekuwa hivyo kutokana na ubora wa Azam hasa tunapokutana nao.
“Tulihitaji zaidi kupata pointi tatu katika mchezo huu ambazo zingetufanya kupunguza tofauti ya pointi iliyopo. Tulitengeneza nafasi za kadhaa za kufunga lakini hatuwa na bahati.
“Kuna nafasi tulipata kipindi cha kwanza Pape Sakho alipiga shuti likagonga mwamba, kipindi cha pili tulijitajidi kucheza lakini hatukubadili matokeo,” amesema Pablo.