Kocha Mkuu Pablo Franco ameweka wazi kuwa mashabiki wana mchango mkubwa kwa timu hasa katika michuano ya klabu Afrika.
Pablo amesema mashabiki wetu wanachangia kwa kiasi kikubwa ushindi unaopatikana hasa katika michuano hii ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Kwa kutambua umuhimu huo, Pablo amewaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi Jumapili katika mchezo dhidi ya US Gandarmerie ambao tunauchukulia kama fainali.
“Mashabiki wamekuwa wa moto hasa katika michuano hii ya Kombe la Shirikisho Afrika. Mchango wao ni mkubwa hasa katika mechi za nyumbani.
“Mashabiki ni watu muhimu kwa ushindi wa timu, niwaombe wajitokeze kwa wingi Jumapili naamini tutapata ushindi,” amesema Pablo.
2 Responses