Pablo: Mechi dhidi ya Namungo itakuwa nzuri

Kocha Mkuu Pablo Franco, amesema mchezo wa kesho wa Nusu Fainali ya Michuano ya Mapinduzi dhidi ya Namungo FC utakuwa mzuri wa kuvutia kuutazama.

Pablo amesema timu zote zinacheza mpira wa chini usiokuwa na matumizi makubwa ya nguvu kama ilivyokuwa katika michezo iliyopita.

Pablo ameongeza kuwa anaamini waamuzi watachezesha vizuri kwa kufuata sheria zote 17 za soka bila kuwalinda wanaocheza rafu hasa zile zinazohatarisha afya za wachezaji.

“Mchezo utakuwa mgumu, Namungo ni moja ya timu nzuri. Tunaamini itakuwa mechi bora ya kutazama kwa kuwa timu zote zinacheza soka na si vurugu.

“Michuano inapofika katika hatua hii kila mechi inakuwa ngumu na tumejiandaa kwa hilo. Changamoto ni kuwa hakuna muda wa kutosha kuandaa timu hivyo katika mazoezi ya leo tutajua wachezaji gani tutawatumia kesho,” amesema Pablo.

Kwa upande wake nahodha msaidizi, Shomari Kapombe amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri na wanafahamu mchezo utakuwa mgumu lakini wapo tayari kupambana kutafuta ushindi.

“Tunahitaji kuingia fainali ya michuano hii na hatimaye tuchukue ubingwa. Namungo tunawajua ni timu nzuri na tumetoka kucheza nao wiki chache zilizopita lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda,” amesema Kapombe.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER