Pablo: Mechi dhidi ya Mbeya City itakuwa ngumu

Kocha Mkuu Pablo Franco, ameweka wazi kuwa mchezo wetu wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mbeya City utakuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani na aina ya uwanja tutakaotumia.

Pablo amesema tutaingia katika mchezo huo kwa tahadhari zote ili kuhakikisha tunaondoka na alama zote tatu.

Pablo ameongeza kuwa baada ya mazoezi ya mwisho ya leo jioni ndio atafahamu wachezaji gani watakuwa tayari kwa mchezo wa kesho.

“Mchezo utakuwa mgumu, Mbeya City ni timu bora, tunaenda kucheza kwenye uwanja ambao hautaturuhusu kucheza mpira wa chini. Tunahitaji kuwa makini na mipira ya kutengwa ili tuwe salama,” amesema Pablo.

Kwa upande wake Nahodha Msaidizi Shomari Kapombe, amesema tunahitaji kufanya vizuri kesho ili kuendelea tulipoishia baada ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi.

“Tumetoka kushinda Mapinduzi, tunapaswa kushinda kesho ili kuendeleza morali ya kufanya vizuri kwenye ligi,” amesema Kapombe.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER