Kocha Mkuu Pablo Franco, amesema mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Polisi Tanzania utakaopigwa Uwanja wa Ushirika utakuwa mgumu kwetu kutokana na kutopata maandalizi ya kutosha.
Pablo amesema kikosi kimewasili Moshi jana kutoka Tanga kilipocheza mechi ngumu dhidi ya Coastal katika uwanja ambao haukuwa rafiki na kesho kinacheza tena kwenye mazingira kama yale bila kupata muda wa kutosha wa mazoezi.
Pablo ameongeza kuwa kutokana na kubana kwa ratiba na kucheza katika viwanja vya aina hiyo kuna hatari ya kuendelea kupata wachezaji majeruhi.
“Mchezo utakuwa mgumu zaidi kwetu, hatujapata muda wa kufanya mazoezi. Tumesafiri jana kwa basi kuja hapa tukitoka Tanga na kesho tunatakiwa kucheza.
“Tumecheza katika uwanja wa kawaida juzi na kesho itakuwa hivyo hivyo, ni hatari sana kwani tunaweza kuongeza idadi ya majeruhi,” amesema Pablo.