Pablo: Malengo yetu yametimia

Kocha Mkuu Pablo Franco, amesema amefurahi timu kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwani ndiyo yalikuwa malengo yetu.

Pablo amesema tuliingia kwenye mchezo wa leo na mbinu za kuhakikisha hatuwapi nafasi ya kutufunga mapema kwani wangetutoa mchezoni kitu ambacho tulikimudu hadi dakika 10 za mwisho kuelekea mapumziko.

Pablo akizungumzia mchezo huo amesema tuliwapa Red Arrows nafasi ya kumiliki mpira nasi kushambulia kwa kushtukiza ili tupate bao la mapema ambalo lingewawatoa mchezoni kwa kuwa tulikuwa na mtaji mzuri wa mabao.

“Tulitaka kutafuta bao la mapema ambalo lingewachanganya wapinzani, mwanzoni tulipata nafasi mbili kubwa zile za Hassan Dilunga ambazo kama tungefunga tungemaliza mechi mapema.

“Lakini nimefurahi kwa matokeo haya kwa kuwa malengo yetu yalikuwa kufuzu hatua ya makundi na tumefanikiwa, tunajua mashindano haya ni magumu kadiri unavyosonga mbele lakini tutajipanga ili kuendelea kufanya vizuri,” amesema Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER