Kocha Mkuu Pablo Franco na kiungo mshambuliaji Clatous Chama, wame wameng’ara katika Tuzo za Ligi Kuu ya NBC za mwezi Machi.
Pablo amechaguliwa Kocha Bora wa Ligi wa Mwezi wakati Chama akishinda Tuzo ya Mchezaji Bora.
Pablo amewashinda Kocha wa Yanga, Nasreddine Al Nabi na Francis Baraza wa Kagera Sugar ambao aliingia nao fainali ya kinyang’anyiro hicho.
Kwa upande wake Chama amewashinda (kina nani) ambao ameingia nao fainali katika kinyang’anyiro hicho.
Hii ni mara ya kwanza kwa Pablo kushinda tuzo hiyo tangu ajiunge nasi klabuni na kwa upande wa Chama pia baada ya kurejea tena kikosini Januari.