Pablo awasifu wachezaji ushindi wa KMC

Kocha Mkuu Pablo Franco, amewasifu wachezaji wetu kwa jinsi walivyojituma na kufanikiwa kupata ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya KMC katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora.

Pablo amesema ushindi wa leo ni muhimu sana kama vile tumetwaa ubingwa kwa sababu wachezaji walijitoa kwa nguvu ingawa hatupata muda wa kujiandaa.

Pablo ameongeza tulicheza vizuri dakika 25 za kwanza lakini baadaye tukapoteza umiliki wa mchezo kabla ya kurejea kipindi cha pili na kuongoza mchezo.

“Kwangu mimi wachezaji ni mashujaa, walifanya kila kitu kilichotakiwa. Ushindi huu ni muhimu kwangu kama tumetwaa ubingwa. Walicheza kama Simba wanavyotakiwa kucheza.

“Hatukuwa tumepata muda wa kufanya maandalizi kutokana na wachezaji wengi kuugua lakini tulipambana muda wote hadi tukapata ushindi, nimefurahi sana kwa matokeo ya leo,” amesema Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER