Pablo awamwagia sifa wachezaji

Kocha Mkuu Pablo Franco, amewasifu wachezaji wetu kwa kiwango safi na kujituma muda wote katika mchezo wa leo wa Ligi Kuu dhidi ya Yanga.

Pablo amesesema wachezaji walijitoa kwa hali zote kuhakikisha tunapata ushindi kitu ambacho kimemfanya kujivunia kufanya nao kazi.

Ameongeza kuwa licha ya kupata siku mbili za kufanya mazoezi baada ya kurudi kutoka Zambia lakini wachezaji walijitahidi kufuata maelekezo.

“Najivunia kufanya kazi na wachezaji hawa, wamefanya kazi kubwa kila mmoja alitimiza vema majukumu yake uwanjani.

“Siwezi kumsifu mchezaji mmoja mmoja bali ni timu nzima, tulizuia kwa pamoja na kushambulia kwa pamoja kilichokosekana ni bao la ushindi tu,” amesema Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER