Pablo ataja mbinu zilizoimaliza Berkane

Kocha Mkuu Pablo Franco, amesema tuliamua kutumia udhaifu wa RS Berkane hasa upande wa kushoto kuanzisha mashambulizi ambayo yaliwafanya kuwa na wakati mgumu muda wote.

Pablo amesema tulihakikisha hatuwapi nafasi kwa mipira ya kutenga kwa kuweka watu wa kuzuia ambapo tuliwafanya kukosa mbinu mbadala na kutufanya kuwa salama zaidi.

“Niliamua kumuanzisha Kibu Denis kwa ajili ya kusaidia kushambulia na kukaba kutokana na uwezo wake licha ya kutoka majeruhi na hakupata muda mrefu wa kucheza.

“Lakini pia udhaifu wao hasa upande wao kushoto ulitusaidia kuutumia na tukafanikiwa. Tuliweka wachezaji ambao wanaweza kuzuia mipira yao ya kutenga na tulifanikiwa muda mwingi wa mchezo,” amesema Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER