Pablo amewapongeza wachezaji ushindi wa Kagera

Kocha Mkuu Pablo Franco amewasifu wachezaji kwa kufanikisha kupatikana kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar uliopigwa jana Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Pamoja na kuwasifu wachezaji kwa ushindi huo Pablo amesema tulistahili kupata ushindi mnono zaidi kama tungetumia vizuri nafasi tulizopata.

Pablo amesema tulicheza vizuri kipindi cha kwanza na kutawala mchezo na kutengeneza nafasi lakini kipindi cha pili hatukuwa bora sana katika kuzitumia.

“Nawapongeza wachezaji kwa ushindi huu muhimu, walijitahidi kupambana kwa ajili ya timu. Lakini kipindi cha pili hatukuwa bora sana katika kutumia nafasi tulizopata ambazo zingetufanya kupata ushindi mnono zaidi.

“Henock Inonga amecheza kama kiungo mkabaji sababu wachezaji watatu katika nafasi hiyo ni majeruhi. Tuna idadi kubwa ya wachezaji wa kikosi cha kwanza ambao ni majeruhi kutokana na ugumu wa ratiba,” amesema Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER