Pablo ajipanga kivingine mechi na Ruvu

Kuelekea mchezo wetu wa kesho wa hatua ya 16 bora ya Michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Ruvu Shooting, Kocha Mkuu Pablo Franco amesema tutaingia kivingine kutokana na hali ya kikosi kilivyo.

Pablo amesema baada ya mchezo wetu wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya ASEC Mimosas kuna baadhi ya wachezaji walipata maumivu hivyo hawatakuwa sehemu ya mechi ya kesho.

Pablo ameongeza kuwa anategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Ruvu na mchezo utakuwa mgumu lakini licha ya kukosa muda wa maandalizi tunahitaji kushinda ili tufuzu hatua inayofuata.

“Kutakuwa na mabadiliko kidogo ya kikosi na tutaingia kivingine, baada ya mechi ya juzi hatujapata muda wa kuweka miili sawa (recovery) lakini tunahitaji kushinda.

“Tulikuwa katika kiwango bora kwenye mchezo uliopita. Tunakwenda kukutana na timu bora na hii ni mechi ya mtoano kwa hiyo tunapaswa kuhakikisha tunakuwa makini, ni muhimu kwetu kuingia hatua inayofuata,” amesema Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER