Pablo ajiamini kuwamaliza Red Arrows

Kocha Mkuu Pablo Franco, amesema anaamini tutaibuka na ushindi katika mchezo wetu wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Red Arrows kutoka Zambia utakaofanyika Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa kutokana na maandalizi tuliyofanya.

Pablo amesema wachezaji wanaelewa haraka mafunzo anayowapa na wanazidi kuimarika siku hadi siku kitu ambacho kinampa matumaini ya kuibuka na ushindi.

Pablo amekiri mchezo utakuwa mgumu zaidi ya ule wa Jwaneng Galaxy lakini kikosi kipo kamili kuhakikisha tunapata ushindi katika uwanja wa nyumbani.

“Kuelekea mchezo huo kutakuwa na mabadiliko kadhaa ya kikosi kitakachoanza kutokana ubora wa wachezaji wanaoonyesha mazoezini.

“Wachezaji wamekuwa wakiimarika siku hadi siku, katika kipindi hiki kifupi nilichokuwa nao wameonyesha ukomavu mkubwa na ninaamini tutapata ushindi.

“Tunafahamu mechi itakuwa ngumu zaidi hata ile ya Jwaneng lakini tumejiandaa kucheza nyumbani ili kupata ushindi. Kutakuwa na mabadiliko ya kikosi sababu tuna wachezaji 34 na wote wako tayari kwa mchezo,” amesema kocha Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER