Pablo aanza kazi Simba

Kocha Mkuu Pablo Franco, leo ameanza rasmi kukiongoza kikosi chetu katika mazoezi yake ya kwanza tangu ajiunge nasi.

Kocha Pablo ametua nchini juzi kutoka Hispania na moja kwa moja ameanza majukumu yake akisaidiwa na wasaidizi wake Seleman Matola na Hitimana Thierry.

Kikosi chetu kinafanya mazoezi katika Uwanja wa Boko Veterans kujiandaa na mchezo ujao wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting utakaopigwa Novemba 19 Mkoani Mwanza.

Wachezaji waliopo mazoezini ni wale ambao hawajaitwa katika timu zao za taifa zinazojiandaa na mechi za kufuzu Fainali za Kombe la Dunia.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER