Tumefanikiwa kupata saini ya miaka miwili ya mshambuliaji Pa Omar Jobe raia wa Gambia kutoka klabu ya FC Zhenis inayoshiriki Ligi Kuu nchini Kazakhstan.
Nchini Gambia PA Omar anajulikana kwa jina la utani la Drogba. Moja ya rekodi yake ni kuwa mfungaji bora wa ligi ya Senegal akicheza pamoja na Babacar Sarr kwenye ligi hiyo kabla ya kwenda Ulaya.
Idara ya ushambuliaji ni moja ya eneo ambalo Kocha Mkuu Abdelhak Benchikha alitaka tulifanyie maboresho na ndio tumefanikiwa kumleta Jobe.
Jobe anakuwa mchezaji wa pili wa Kimataifa kusajiliwa katika dirisha hili la usajili baada ya Babacar Sarr ambaye tumemsajili kutoka US Monastir ya Tunisia.
Nyota wengine tuliowasajili katika dirisha hili la usajili ni Salehe Karabaka kutoka JKU na Ladack Chasambi.