Opa kupaa Uturuki kufanya majaribio

Mshambuliaji wetu kinara wa Simba Queens, Opa Clement ataondoka leo usiku kuelekea nchini Uturuki kwa ajili ya kufanya majaribio katika timu ya Kayserispor Girl.

Majaribio hayo yatakuwa ya mwezi mmoja na endapo atafanya vizuri Kayserispor watakuja mezani kujadiliana nasi kabla ya kumsajili moja kwa moja.

Baada ya kupata nafasi hiyo, Opa ameushukuru uongozi wa klabu kwa kumkubalia kwenda kufanya majaribio na anaamini ndoto zake za kucheza soka la kulipwa nje ya nchi inatimia.

“Naushukuru uongozi wa klabu kwa kuniruhusu kwenda kufanya majaribio. Ndoto yangu ni kucheza soka la kulipwa nje ya nchi pia nataka kuwa balozi mzuri wa Simba na nchi kwa ujumla kama nitafanikiwa,” amesema Opa.

Kama Opa atafanya vizuri na kufanikiwa kufuzu majaribio atakuwa mchezaji wa pili kutoka kikosi chetu kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi baada ya Mwanahamisi Omary ambaye anakipiga nchini Morocco.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER