Uongozi wa klabu ya Simba umefikia makubaliano ya kumuuza nahodha wa timu yetu ya Simba Queens, Opa Clement kwenda Besiktas ya Uturuki.
Tayari mshambuliaji huyo kinara ameshaondoka nchini kuelekea Uturuki kwenda kuanza maisha mapya ya soka katika timu yake ya Besiktas.
Mpaka Opa anaondoka Ligi ya Wanawake (Serengeti Lite Women’s Premier League) mzunguko wa kwanza umemalizika na yeye ndiye kinara wa ufungaji akiwa amepachika wavuni mabao tisa.
Uongozi wa Klabu ya Simba unamtakia Kheri Opa katika majukumu yake mapya na pia una mkaribisha muda wowote atakapoamua kurejea tena nyumbani.